JEMBE:BWALYA MAJI KUPWA MAJI KUJAA,

MCHAMBUZI wa Soka Saleh Ally ‘Jembe’ katika kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na 255globaradio na Global TV amesema kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia Rally Bwalya amekuwa kwenye kiwango ambacho hakieleweki kwa kukipa tafsiri ya maji kupwa maji kujaa.

Jembe amesema kwamba kuna muda anakuwa katika kiwango kizuri na muda mwingine anakuwa kwenye kiwango kibovu.

Jembe amedai kwa kipindi alichoondoka Clatous Chama kwenda RS Berkane ya nchini Morocco Rally Bwalya alitegemewa kuwa mtu ambaye angeweza kurithi mikoba ya kiungo huyo mchezeshaji ambaye naye ni raia wa Zambia, lakini alishindwa.

Ingawa Chama naye amerudi kwa mara nyingine ndani ya viunga vya Msimbazi hali kwa Bwalya imeendelea kuwa ile ile mara nyingi ameonekana kuwa mzuri pale ambapo klabu yake inacheza na timu dhaifu au pale ambapo haihitaji zaidi msaada wake.

Hadi sasa klabu ya Simba ina jumla ya alama 50 alama 10 nyuma ya vinara Yanga wenye alama 60 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC huku timu zote zikiwa zimebakiwa na michezo 6 tu hadi kukamilika kwa Ligi.