COASTAL UNION YAINYOOSHA DODOMA JIJI,NAMUNGO,PRISONS HAKUNA MBABE

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Mei 20 umeendelea ambapo mechi mbili zimekamilika kwenye viwanja viwili tofauti.

Mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ubao umesoma Coastal Union 2-1 Dodoma Jiji.

Mabao ya Coastal Union mtupiaji ni kijana Abdul Suleiman aliyeanza kuwatungua Dodoma Jiji dk 7 na 15 lile la Dodoma Jiji ni mali ya Anuary Jabir dk ya 23.

Ule mwingine uliochezwa Uwanja wa Ilulu, Lindi ubao umesoma Namungo 3-3 Prisons.

Ni mabao ya Haruna Shamte dk 5, Nurdin Chona yeye alijifunga dk ya 65 na msumari wa mwisho ulifungwa na Lukas Kikoti ilikuwa dk ya 86.

Kwa Tanzania Prisons ni mabao ya Ezekiel Mwashilindi dk ya 8,Jumanne Elifadhil dk ya 56 na Moses Kitandu dk ya 77.