BOSI SIMBA,YANGA WAITWA KAMATI YA MAADILI TFF

OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez atafikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa ushahidi wa shutuma anazodaiwa kuzitoa wakati akihojiwa na Kituo cha Radio  nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa, Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko yao kwa TFF dhidi ya Barbara ikidai kuwa ali Barbara akihojiwa na radio hiyo alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya Yanga.

Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba inamlalamikia Msemaji wa Yanga, Haji Manara kwa madai kuwa kupitia matandao wa kijamii alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya Klabu yao.

Baada ya kusikiliza malalamiko hayo mwenyekiti wa kamati ya maadili alielekeza Sekretarieti ya TFF kuhakikisha walalamikiwa wote wamepewa mashtaka dhidi yao pamoja na mwito wa kuhudhuria mashauri hayo ambayo yataanza kusikilizwa Mei 14, 2022.