MEI 18, Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa timu kuzidi kusaka ushindi kwenye mechi ambazo watacheza na leo ni mchezo mmoja tu wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa.
Azam FC itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.
Azam FC ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 32 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 49.
Unakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-1 Azam FC.
Kwa mechi ambazo zilichezwa jana Mei 17 matokeo yalikuwa namna hii:-
Mbeya Kwanza 0-1 Geita Gold, mtupiaji wa bao alikuwa ni George Mpole dk ya 12.
Biashara United 1-2 Namungo FC, mabao yote mawili kwa Namungo yalfungwa na Shiza Kichuya ilikuwa dk ya 9 na 67 na lile la Biashara United lilifungwa na Ambrose Awio ilikuwa dk ya 85.