MSHINDI wa Jacpot Florian Valerian Massawe amekabidhiwa mfano wa hundi ya Bilioni 1,255,316,060/ na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Tarimba Abbas.
Ni leo Mei 18 mshindi huyo amekabidhiwa katika ofisi za Sportpesa mbele ya mwakilishi kutoka TRA, Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Michezo ya Kubahatisha pamoja na mke wa mshindi Lightness Florian Massawe.
Mshindi huyo amesema kuwa ushindi huo ni furaha kwake kwa kuwa alikuwa anachukulia kama kazi kubashiri michezo na mke wake alikuwa meneja wake.
Ni usafiri wa Helkopta ulimfuata bilionea huyo mpya na kumleta makao makuu ya ofisi za SportPesa.