WASHIKA BUNDUKI WAMECHANA MKEKA

KICHAPO cha mabao 2-0 wakiwa ugenini kimewapunguza kasi washika bunduki kuigusa Top 4 kutokana na kuachwa pointi na wale walio nafasi ya nne.

Ni Tottenham ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 37 ikiwa ni tofauti ya pointi mbili na Arsenal.

Ben White alijifunga dk ya 55 ya mchezo ilikuwa ni kipindi cha pili baada ya zile dk 45 za mwanzo ngoma kuwa ngumu kwa pande zote mbili.

Msumari wa pili ulipachikwa na Bruno Guimaraes ilikuwa dk ya 85 na iliwapa nguvu vijana hao kuweza kushinda mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali.

Katika Uwanja wa St James Park vijana wa Newcastle United walibakisha pointi zote tatu muhimu zinazowafanya wafikishe pointi 46 wakiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo.

Arsenal wao wanabakiwa na pointi zao 66 na wapo ndani ya tano bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.