>

MBWANA MAKATA,MENEJA WA MBEYA KWANZA WAFUNGIWA

KOCHA wa Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na Meneja wa timu hiyo, David Naftali, wamefungiwa kwa kipindi cha miaka mitano (5) kila mmoja kwa kosa la kushawishi/kuamuru wachezaji wasiingie uwanjani kuanza mchezo,

 Tukio hilo lililosababisha Mechi Namba 180 ya Ligi Kuu Bara Namungo vs Mbeya Kwanza usichezwe lilitokea kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imeeleza kuwa kitnedo hicho kilikuwa ni kinyume na kanuni na kimesababisha hasara.

Kutokana na suala hilo Namungo FC imepewa alama tatu na mabao matatu za mchezohuo ambao ulipaswa kuchezwa Mei 13.

Sababu kubwa ya Mbeya Kwanza kugomea mchezo huo ni kile walichoeleza kuwa kanuni za mchezo hazikukamilika kwa kuwa gari la kubebea wagonjwa , (Ambbulace) haikuwepo.

Taarifa iliyotolewa na Kamshina wa Mchezo huo imeeleza kuwa Ambulance ilikuwepo lakini ilitoka muda mfupi baada ya kupata dharula ya mgonjwa na ilirejea saa 10:23 ikiwa ni muda ambao walipaswa kuanza mchezo.

Kocha na Meneja wao walikuwa wanasimamia kanuni kwamba mchezo ulipaswa kusimama kwa kuwa ni dk 15 ambazo walikuwa wanasimamia.

Leo Mbwana Makata yupo kwenye benchi akiongoza mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza v Geita Gold.