>

KATWILA ATAJA KILICHOWAREJESHA LIGI KUU BARA

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa kurejea kwao ndani ya Ligi Kuu Bara kumetokana na mipango mizuri iliyopangwa pamoja na ushirikiano kutoka kwa wachezaji.

Ihefu ilishuuka ndani ya ligi msimu uliopita wa 2020/21 na sasa umerejea ndani ya ligi kwa ajili ya kuendelea na ushindani kwa mara nyingine tena.

Katwila ameweka wazi kwamba anatambua ushindani wa ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi hivyo nao watapambana.

“Kupanda kwetu ligi ni faraja na ilikuwa kwenye mpango wetu hivyo ambacho tunakifanya ni kuwa kwenye mwendelezo mzuri wakati ujao.

“Tunatambua kwamba ligi ni ngumu ipo wazi nasi tutafanya jitihada kubwa kupata matokeo kwa mechi ambazo tutacheza msimu ujao,” amesema.

Ni timu mbili kutoka Championship zimeweza kupanda ikiwa ni pamoja na DTB