GEITA GOLD YAITUNGUA MBEYA KWANZA,MPOLE ATUPIA

GEITA Gold imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

Katika mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa mapema kabisa mshambuliaji namba moja wa Geta Gold,George Mpole aliweza kupachika bao la kuongoza.

Mpole ambaye ni mpole kwenye maana ya jina lakini kwenye kucheka na nyavu hana huruma aliweza kupachika bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa leo Mei 17.

Anafikisha mabao 13 akiwa ni namba moja kwa utupiaji anafuatiwa na Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 12 kibindoni.

Inafikisha jumla ya pointi 34 na kuishusha Azam FC nafasi ya tatu na kukaa hapo kwa muda msimu wa 2021/22.

Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 21 ikiwa nafasi ya 16 pia kwenye mchezo wa leo Enock Jiah wa Mbeya Kwanza aionyeshwa kadi mbili za njano na kupelekea kuonyeshwa kadi nyekundu.