FAINALI KUPIGWA ARUSHA,YANGA NA SIMBA MWANZA

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Simba wanatarajia kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Mei 28.

Yanga walikuwa wa kwanza kuweza kukata tiketi kwa ushindi mbele ya Geita Gold kisha Simba wakafuata kwa ushindi mbele ya Pamba kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili.

Mechi zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa na watani hao kuweza kushinda mechi zao.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza majira ya saa 9:30 alasiri.

Azam FC wao watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Coastal Union, itakuwa ni Mei 29, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid itakuwa nusu fainali ya pili.

Mshindi wa nusu fainali ya kwanza atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, itakuwa Julai 2,2022.