PAMBA YATAKA KUITIBULIA SIMBA

KOCHA Msaidizi wa Pamba, Yangoo Mamboleo amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini wataingia kwa tahadhari ili kuweza kushinda.

Pamba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Simba ambao nao wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo amao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunatambua kwamba ushindani mkubwa ambacho tutajitahidi ni kutafuta ushindi kwenye mchezo huo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya mchezo huu ambao una ushindani mkubwa na kila mmoja anahitaji ushindi ambao ni muhimu na kila mmoja anahitaji ushindi.

“Kwa ambacho kipo kwa wakati huu ukweli ni kwamba kila mmoja anahitaji kushinda nasi tunahitaji ushindi washindani wetu tunawaheshimu hivyo wajitokeze kwa wingi mashabiki” amesema.

Mshindi wa mchezo wa leo atatinga hatua ya nusu fainali ambapo atakwenda kumenyana na Yanga iliyoshinda mbele ya Geita Gold.