PABLO ATUMA UJUMBE HUU KWA PAMBA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Pamba.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku na mshindi wa mchezo anakwenda kukutana na Yanga hatua ya nusu fainali.

Pablo amesema kuwa kuna ushindani mkubwa ambao upo kwenye Kombe la Shirikisho na hilo lipo wazi kutokana na timu kuweza kuhitaji ushindi.

“Ukweli ni kwamba kila mmoja anahitaji kuweza kufika mbali jambo ambalo linafanya ushindani kuwa mkubwa, nasi tupo imara na tutaingia kushindana.

“Ambacho tunahitaji ni kuweza kusonga mbele hasa ukizingatia wapinzani wetu wanafanya vizuri huko kwenye Championship hivyo tutaingia kwa hesabu za kupata ushindi,”.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni Simba na walitwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Kikosi cha Simba jana kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo ambapo miongoni mwa nyota waliokuwa katika mazoezi hayo ni pamoja na Sadio Kanoute,Mzamiru Yassin,Kibu Dennis.