MECHI ya Yanga dhidi ya Dodoma Jiji ambayo inatarajiwa kuchezwa Jumapili, Uwanja wa Jamhuri imebadilishwa muda kutoka ule uliopangwa awali.
Awali ilikuwa ni saa 1:00 usiku mchezo huo wa ligi uchezwe na sasa unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.
Sababu za mchezo huo kubadilishwa muda ni kutokana na uwanja huo kuwa na matumizi mengine.
Tayari timu zote zimepewa taarifa kuhusu mabadiliko ya muda wa mchezo huo wa ligi ambao ni wa mzunguko wa pili ndani ya msimu wa 2021/22.