HAJI Manara,Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa mshambulaji wa kikosi hicho Fiston Mayele ni fundi wa kupiga penalti kuliko watu wanavyofikiria.
Kwenye mchezo dhidi ya Prisons Mayele alikosa penalti ya kwanza ndani ya ligi na kuwafanya wakose mazima pointi tatu na kugawana mojamoja Uwanja wa Mkapa.
Manara amesema kuwa kilichotokea kwa Mayele ni jambo ambalo huwa linatokea kwa mchezaji yoyote na hata angepewa mwingine huenda ingetokea hivyo.
“Kilichotokea kwa Mayele ni jambo la kawaida lisitutoe kwenye reli kwani Mayele ni mpigaji mzuri wa penalti na hilo lipo wazi kwa uwa kuna penalti ambazo aliwahi kufunga na hata kabla hajaja huko alikokuwa alikuwa anapiga penalti.
“Labda tuseme kwamba wanasema kwa nini asingepewa Djuma Shaban kwa kuwa yeye huwa anapiga penalti hilo huwa linatokea kwa wachezaji kukosa penalti.
“Kwa namna ambavyo inatokea kwa wachezaji lakini sio mbaya kuona kwamba wanashindwa kufunga hivyo tusitoke kwenye reli lazima tuendelee na mapambano,”.
Mayele ametupia mabao 12 kwenye ligi na ametoa pasi tatu za mabao.