RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

MEI 11,2022 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa pili.

Polisi Tanzania itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji, mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika.

Coastal Union itakuwa na kazi ya kumenyana na Biashara United mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Kagera Sugar ngoma inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa.