AZAM FC imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 mbele ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine.
Nyota wa Mbeya City Juma Shemvuni dakika ya 51 kwenye mchezo huo alipachika bao la kuongoza.
Kwa Azam FC bao pekee la kufutia machozi lilifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 88 kwenye mchezo huo ikiwa ni dakika 5 zimepita kwa beki wao Daniel Amoah kujifunga bao dk ya 83 katika harakati za kuweza kuokoa mpira.
Mabao yote yalifungwa kipindi cha pili kwa kuwa dk 45 za awali ngoma ilikuwa 0-0.
Sasa Azam FC kwenye msimamo inabaki na pointi 32 nafasi ya tatu huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 4 na pointi 31.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex timu hizi mbili ziligawana pointi mojamoja baada ya sare ya kufungana mabao 2-2.
Jana, Mei 11,Azam FC iliweza kuyeyusha pointi tatu mazima mbele ya Mbeya City ikiwa ugenini.