YANGA YAKWAMA MBELE YA TANZANIA PRISONS

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi wamekwama kusepa na pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Hata Prisons nao wamekwama kupata pointi tatu zaidi ya kuambulia pointi moja wakiwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Kwenye msimamo Prisons ipo nafasi ya 14 na pointi 23 baada ya kucheza mechi 23.

Baada ya dakika 90 kukamilika Mei 9,hakuna timu ambayo iliweza kucheka na nyavu kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi kubwa.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele katika mchezo huo alikosa penalti baada ya kupaisha na kufanya ashindwe kufikisha bao la 13 ndani ya ligi.

Ilikuwa ni dk ya 38 ya kipindi cha kwanza Yanga walipata penalti ila ilishindwa kuwapa bao la kuongoza kwa kuwa mpigaji hakuwa na bahati.

Anabakiwa na mabao yake 12 akiwa sawa na George Mpole wa Geita Gold ambaye huyu ni mzawa.

Inakuwa ni sare ya sita kwa Yanga wenye pointi 57 wakiwaacha kwa pointi 11 wapinzani wao wa kariu Simba ambao wapo nafasi ya pili na pointi 46.