SIMBA YASIMULIA MATESO YA DAKIKA 270

SELEMAN Matola,Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wamekuwa kwenye mwendo usiofurahisha kwenye mechi tatu mfululizo jambo wanalolifanyia kazi.

Kwenye mechi hizo tatu za ligi ambazo ni dakika 270 katika msako wa pointi 9 waliambulia pointi tatu pekee na kuacha mazima pointi 6 ambazo ni mateso kwao huku wakifungwa mabao mawili sawa na yale ambayo walifunga.

 Matola amesema kuwa kwenye mechi tatu mfululizo hawakupata matokeo waliyokuwa wanayatarajia jambo ambalo wanalifanyia kazi.

“Tumecheza mechi tatu za ligi bila kupata matokeo hilo sio jambo ambalo tulikuwa tunahitaji tunalifanyia kazi hasa kwenye uwanja wa mazoezi ili kuweza kupata ushindi.

“Ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, (0-0),Yanga, (0-0) na Namungo, (2-2) hatujapenda kuona inakuwa hivi tuna amini kwamba kwa mechi ambazo zimebaki kutakuwa na mabadiliko na tutafanya vizuri,” amesema.

Waliibuka kwenye mechi ya nne mbele ya Ruvu Shooting kwa ushindi wa mabao 4-1 Uwanja wa Mkapa.