BECKHAM AMZUIA RONALDO KUONDOKA UNITED

STAA mkongwe wa soka, David Beckham amesema anatamani kuona staa wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anasalia kikosini hapo kwani ni mchezaji muhimu.

Hii ni baada ya kuwepo tetesi kuwa huenda Ronaldo akatimka kikosini hapo, baada ya Man United kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, licha ya kuwa na mkataba wa mwaka mmoja

Man United imekuwa katika wakati mkubwa baada ya kushindwa kutamba kabisa katika msimu huu wa 2021/22 katika michuano yote.

Beckham ambaye ni moja kati ya mastaa wa Class of 92 ya Man United, alisema ni muhimu Ronaldo kubaki kikosini hapo kwani klabu hiyo ina maana kubwa.

“Ukweli Cristiano ni moja kati ya wachezaji bora kwa zaidi ya miaka 15 yeye na Leo (Messi). Matumaini yangu ni kuona anabaki ndani ya United ni muhimu kwa mashabiki wa klabu na ina umuhimu kwake pia kwani tunajua jinsi gani United kwake ina maana.

“Najua ataendelea kuwa bora kama alivyosasa kwa kufunga mabao na kutengeneza na hakuna asiyejua ubora wa Cristiano kwa Man United bila kujali umri wake amekuwa akipambana kufanya vizuri.

“Nafahamu wamepita katika msimu mgumu na ndiyo huo umemalizika, lakini mashabiki watamshukuru kwa kile alichokifanya kwani amepambana licha ya kupitia magumu na siku zote hali kama hiyo haikwepeki.”

06

Beckham alitwaa mataji sita ya Premier League akiwa na Man United.