MECHI 100 kwa Shomari Kapombe akiwa na Simba tokea 2018 ni kazi kubwa ambayo ameifanya mkongwe huyu mwenye uwezo wa kupanda na kushuka.
Yes, kwanza tuwapongeze Simba angalau kukumbuka wana mchezaji amecheza mechi idadi hiyo.
Kwa kufanya hivyo itawaumbusha na wengine waweze kutambua kwamba kuna wachezaji wao wamecheza mechi ngapi na itawapa heshima kutamua mchango wao.
Mechi 100 kwa Kapombe zimekuwa na manufaa makubwa na mfano wa kuigwa.
Ndiye beki bora zaidi kwa misimu mitano mfululizo na wazalendo wana sehemu ya kujifunza kabla ya kuwaangalia wachezaji wa kigeni.
Kwa Afrika Kapombe kakutana na wachezaji wa level zote na level za ukubwa wa timu zote kubwa na alionyesha uwezo mkubwa.
Hongera Baba Ester ikumbukwe kwamba mchezo wake mbele ya Ruvu Shooting aliweza kuanza akiwa ni nahodha kabla ya John Bocco kuingia kuchukua kitambaa kwa beki huyo mpole.