IKIWA Uwanja wa Mkapa kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2021/22 Simba inapata ushindi mkubwa kwenye mechi za ligi kwa kushinda mabao 4-1 mbele ya Ruvu Shooting.
Awali ilikuwa inashikilia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting kuwa ni mkuwa kwao kwa msimu huu ndani ya ligi baada ya kucheza mechi 22 huku ikivunja ule mwiko wa kutopata matokeo chanya kwenye mechi zake za ligi.
Ikumbukwe kwamba mabingwa hao watetezi walicheza jumla ya mechi tatu mfululizo kwenye ligi bila kuambulia ushindi mpaka pale walipopata kushinda mbele ya Ruvu Shooting.
Ni Kibu Dennis alianza kutupia ilikuwa dk ya 39 Uwanja wa Mkapa,Rally Bwalya alipachika bao la pili dk ya 66,John Bocco alipachika bao la tatu dk ya 81 na Henock Inonga alipachika bao la nne dk ya 83hawa waliweza kutupia kwa upande wa Simba.
Bao la Haruna Chanongo likiwa pekee kwa upande wa Ruvu Shooting ambayo ilicheza kwa umakini mkubwa ilikuwa ni dk ya 83.
Sasa Simba inafikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 22 kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili huku Ruvu Shooting ikibakiwa na pointi 22 nafasi ya 13.