MASTAA watatu wa kikosi cha Simba ndani ya msimu wa 2021/22 kwenye ligi wanapata tabu kwa kuwa wamekwama kufunga kwenye mechi zao zote walizocheza.
Simba wakiwa ni mabingwa watetezi eneo la ushambuliaji wanateswa na tatizo la kushindwa kumaliza nafasi ambazo wanazitengeneza jambo linalowafanya wawe kwenye mwendo wa kusuasua.
Washambuliaji wake watatu msimu huu kwenye ligi hakuna hata mmoja ambaye ameweza kufunga bao kati ya 25 ambayo wamefunga baada ya kucheza mechi 21.
Staa wao namba moja ni John Bocco mtetezi wa kiatu bora cha ufungaji ambapo msimu uliopita alitupia mabao 16 na pasi mbili, msimu huu akiwa amecheza mechi 16 na kuyeyusha dk 639 bado hajafunga wala kutoa pasi ya bao.
Namba mbili ni Chris Mugalu ambaye msimu wa 2020/21 alifunga mabao 15, msimu huu akiwa amecheza mechi 9 na kutumia dk 556 hajafunga zaidi ya kutoa pasi moja mbili za mabao.
Ingizo jipya, Yusuph Mhilu kutoka Kagera Sugar huyu kacheza mechi 10 na kuyeyusha dk 316 bila kufunga wala kutoa pasi ya bao.