HIZI HAPA KUSHUKA UWANJANI LEO BONGO

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea le Mei 8 ambapo kutakuwa na msako wa pointi tatu kwa timu nne kwenye viwanja viwili tofauti ndani ya dk 90 za kazi.

Ni Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda watakuwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu,Malale Hamsini.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wanaonolewa na Kocha Mkuu Pablo Franco watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting ya Masta Mkwasa

Vinara wa ligi ambao ni Yanga wao kesho wanatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons.