CHAMPIONSHIP KITAWAKA LEO

JKT Tanzania leo itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa Championship unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Highland Estate.

Kwenye msimamo JKT Tanzania inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 47 kwenye michezo 27.

Ihefu ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 59 na imecheza pia michezo 27 ndani ya Championship.

Vinara ni DTB ambao wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 62 kibindoni wao watasaka ushindi mbele ya Pamba FC.

Pia mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mwadui FC itakayokaribishwa na Pan African.

Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.