SOKA LA UFUKWENI LINAZIDI KUSHIKA KASI

LIGI ya Soka la Ufukweni inaendelea kushika kasi ambapo kila timu imekuwa ikifanya yake kwenye msako wa pointi tatu.

Jana Mei 7,2022 timu nne zilikuwa uwanjani kusaka ushindi kwenye mechi ambazo walicheza huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi.

Ni kwenye Viwanja vya Fukwe za Coco Beach ambapo wachezaji hao wanasaka ushindi ili kuweza kufikia malengo yao.

Global TV na Global Radio wanadhamini ligi hiyo ambayo imekuwa ikipata umaarufu taratibu kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakijitokeza.

Mchezo uliowakutanisha Savvanah Boys 3-2 Friends Of Mkwajuni,Ilala United 8-5 Dar Footbal Center na PCM Buza 3-9 Vingunguti Kwanza huu ulikuwa ni wa kundi A.

Kwa kundi B ilikuwa Mshikamano City 4-4 Mburahati na mshindi alipatikana kwa penalti ambapo mshikamano ilifunga 1-4 Mburahati.

Bonipace Pawasa, Mratibu wa Ligi ya Soka la Ufukweni amesema kuwa mashabiki waendelee kujitokeza kwa kuwa urudani inatolewa na timu zote zinazoshuka uwanjani.

Dizo_Click.