LEO Mei 7,2022 watatu ni kumbukizi zao za kuletwa duniani wakiwa ndani ya kikosi cha Simba.
Ni mchezaji Erasto Nyoni ambaye ni kiraka huyu msimu huu hajafunga wala kutoa pasi ya bao kwenye mechi za ligi.
Mwingine ni meneja wa timu,Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na familia ya michezo.
Pia mtunza vifaa Hamis Mtambo naye ni siku yake ya kuletwa duniani.
Ikawe kheri katika kutimiza miaka yenu na Mungu awalinde wanafamilia ya michezo.