RATIBA YA LIGI KUU BARA HII HAPA

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo ambapo kuna mechi zitaendelea kwa mzunguko wa pili kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu.

Geita Gold itakuwa na kazi ya kumenyana na Kagera Sugar, Uwanja wa Nyankumbu saa 8:00.

Mtibwa Sugar itakuwa na kazi dhidi ya Mbeya City,Uwanja wa Manungu saa 10:00 jioni.

Azam FC v KMC FC, Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Huu ni mzunguko wa lala salama ambapo ushindani umekuwa ni mkubwa na presha kwa kila timu hivyo wachezaji jukumu lenu kucheza kwa umakini katika kutimiza majukumu yenu.

Waamuzi pia kazi ni kwenu kufuata sheria 17 za mchezo ndani ya dk 90.