AZAM FC YAWAITA MASHABAKI KUIZOMEA KMC

UONGOZI wa Azam FC umewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Azam Complex leo kuwazomea wapinzani wao KMC ili kuwamaliza mapema kwenye mchezo wa ligi.

Timu hiyo ikiwa imetoka kuambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar,leo ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC FC.

 Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kuwazomea wachezaji wa timu pinzani.

“Hatujawa na matokeo mazuri kwenye mechi za hivi karibuni pia kiwango kibaya ambacho tulicheza ni sababu yetu kushindwa kupata matokeo hivyo mashabiki wajitokeze kwenye mchezo wetu ili kuweza kuwashangilia wachezaji wetu na kuwapa wakati mgumu wapinzani kwa kuwazomea.

“Sare dhidi ya Geita haikuwa nzuri kwetu na sisi haturidhiki kwa timu yenye malengo kama sisi na sare na hiyo ni matokeo mabaya kwetu na hatukupata matokeo mazuri Bukoba,” amesema Thabit.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 21.