SARE ZAWAPA HASIRA YANGA

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa matokeo ya sare ambayo wameyapata kwenye mechi za ligi hivi karibuni hayajawatoa kwenye mstari badala yake yamewaongezea hasira ya kuzidi kupambana.

Kwenye mechi mbili mfululizo za ligi mbele ya Simba na Ruvu Shooting vinara hao wa ligi waliambulia pointi mbili katika msako wa pointi 6.

Akizungumza na Saleh Jembe,Kaze amesema kuwa kupata sare kwao ni matokeo mabaya ambayo hawakutarajia lakini hayajawatoa kwenye mstari.

“Tumepata matokeo ya sare haina maana kwamba ni matokeo mazuri kwetu hapana hatujapenda zaidi ya kuweza kuongeza juhudi kwenye mechi zetu zijazo.

“Kushindwa kupata matokeo kunatufanya tuweze kukaa tena kwenye mazoezi na kuzungumza na wachezaji ili kupata matokeo ya kile ambacho tunajifunza na tunaamini kwamba kwa mechi zijazo kutakuwa na mabadiliko,” amesema Kaze.

Kwenye msimamo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 56 baada ya kucheza mechi 22 na haijapoteza mchezo.