BEKI INONGA WA SIMBA APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

BEKI wa Klabu ya Simba inayonlewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco, Henock Inonga leo Mei 6 amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) ya mwezi Aprili.

Tuzo hiyo ameweza kuitwaa baada ya kuwashinda mabeki wenzake ambao ni Shomari Kapombe na Joash Oyango ambao waliingia kwenye fainali ya msako wa mchezaji bora.

 Tuzo ambayo amepewa ni pamoja na mkwaja wa shilingi milioni mbili ambao ni zawadi yake beki huyo kitasa ambaye aliweza kuwika kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Ikumbukwe kwamba mchezo huo uliochezwa Aprili 30 Banka alikuwa na shuguli pevu ya kumzuia Fiston Mayele ambaye alishindwa kufunga katika lango la Simba.

Mayele ni mshambuliaji namba moja kwenye ligi akiwa ametupia mabao 12 na pasi tatu ndani ya msimu wa 2021/22.