ZILE tambo za watani wa jadi Yanga na Simba zimekamilika Uwanja wa Mkapa kwa wababe hao kutoshana nguvu bila kufungana.
Aprili 30, 2022 mwamuzi Ramadhan Kayoko alikamilisha dk 90 bila ubao kusoma mabao kwa kuwa ilikuwa ni Yanga 0-0 Simba.
Sare hiyo ilitawaliwa na matukio ya ubabe mwanzo mwisho ambapo Simba walianza kwa kasi dakika tano za mwanzo kisha Yanga wao wakajibu dakika 5 za mwisho wa kipindi hicho.
Mpaka dakika 90 zinakamilika Yanga haikupiga shuti ambalo lililenga lango ikiwa inamaanisha kwamba walikwenda kujilinda huku Simba ikipiga mashuti mawili ambayo hayakuwa na hatari mikononi mwa kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui.
Ubabe wa Bernardd Morrison ulikuwa mwanzo ila alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo huo wa dabi huku akimuacha mshikaji wake Fiston Mayele akpambana na Henock Inonga.
Yanga inafikisha pointi 55 ikiwa namba moja ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zao ni 42.
Jumla ya mashuti 4 walipiga Simba na hayakulenga lango huku kwa upande wa Yanga yakiwa ni matatu.
Kwa upande wa umiliki Yanga waliweza kumiliki asilimia 49 na wale wa Simba wakimiliki asilimia 51.