MATHIAS Lule, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema malengo ni kuona kikosi hicho kinamaliza ndani ya tano bora kwa msimu huu wa 2021/22.
Ni mechi sita imeshinda kati ya 21 ambazo imecheza kwa msimu huu ndani ya ligi ambao umekuwa na ushindani mkubwa.
Imekusanya pointi 28 ipo nafasi ya 5 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye jumla ya pointi 55 ambazo amezikusanya.
“Malengo yetu ni kuweza kumaliza ligi ndani ya tano bora hilo lipo wazi na tutaweza kupambana ili kupata matokeo kwenye mechi zetu.
“Kwenye mechi zetu ambazo zimepita hivi karibuni hatukuwa na matokeo mazuri lakini haina maana kwamba hatukuwa bora,tuna amini kwa mechi zilizobaki tutafanya vizuri”amesema.
Moja ya mechi ambayo wlishinda kati ya hizo sita ni pamoja na ile mbele ya Simba, Uwanja wa Sokoine kwa bao 1-0 lililofungwa na Paul Nonga.