AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amesema maandalizi ambayo watayafanya kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga utwapa matokeo chanya.
Manula kwenye ligi amekaa langoni katika mechi 16 akiwa ameyeyusha dk 1,440 na ni mabao 7 kafungwa, hajafungwa kwenye mechi 9.
Msimu huu Manula kafungwa bao moja kwa mfungaji kuwa nje ya 18 ilikuwa mbele ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na mtupiaji alikuwa ni Victor Ackpan.
Akizungumza na Saleh Jembe, Manula amesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya uweza kufanya vizuri.
“Ipo wazi kwamba mchezo utakuwa mgumu ila maandalizi ambayo tutayafanya yatatupa nafasi ya kuweza kupata matokeo hivyo ni jambo la kusubiri na kuona itakavyokuwa.
“Baada ya kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa hapo tunaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga na tupo tayari,” amesema Manula.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Manula alikaa langoni na alikuwa shuhuda kwenye sare ya bila kufungana.
Kesho Aprili 30 anapewa nafasi ya kuweza kuanza kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi.