HAJI MANARA ATUPA DONGO KWA SIMBA

OFISA Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba wapo tayari kwa mchezo huo huku wapinzani wao wakiwa ni wa kawada tu.

Kesho Aprili 30,2022 Yanga itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa ligi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji pointi tatu muhimu.

Manara amesema kuwa mchezo huo utawaongezea kasi ya kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 ambao ni malengo yao makubwa.

“Sisi tunatambua kwamba tuna mchezo nao wa ligi wakiwa wametoka kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika ila hao, (Simba) ni wa kawaida tu hatuna mashaka nao hata kidogo.

“Mashabiki tunawahitaji wajitokeze kwa wingi na lengo letu ni kuona kwamba tunaujaza uwanja mapema kwa kuwa uwepo wao utaongeza nguvu kwetu,”.

Kwenye Msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 54 inatarajiwa kumenyana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 41.