ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa kikosi cha Yanga kwa sasa kipo vizuri katika michuano ya ligi kuu jambo ambalo ni hatari kuelekea katika mchezo wa dabi dhidi ya Simba.
Yanga kwa sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 13 dhidi ya Simba wanaoshika nafasi ya pili lakini wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.
“Simba wakipata ushindi katika mchezo huo kuna kitu watapunguza dhidi ya Yanga hivyo kama Simba watashinda litakuwa jambo zuri japo najua lazima wapambane kwa kuwa sio rahisi sana, kushiriki kwa Simba katika michuano ya kimataifa pia ni faida kwa Simba kupata ushindi dhidi ya Yanga.
Rage amesema kuwa Yanga wana kikosi bora na wanafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu jambo ambalo ni kikwazo kwa Simba katika ubingwa wa ligi kuu, hivyo ili kupunguza mzigo wa alama wanatakiwa washinde dhidi ya Yanga ili kujiweka katika nafasi ya kuendelea kuwania ubingwa.
Aprili 30,2022 watani hao wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwenye mchezo wa awali inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 0-0 Yanga.