GUARDIOLA ABAINISHA VINICIUS HAKABIKI

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amebainisha kwamba sio rahisi kumdhibiti Vinicius Jr ila iliwezekana kupitia kwa Fernandinho.

Manchester City ilipata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Uwanja wa Etihad.

Wao City walikuwa ni wenyeji na waliibuka na ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkuwa mwanzo mwisho.

Guardiola amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kuweza kumdhibiti nyota huyo ambaye ana uwezo mkubwa uwanjani wa kufanya kile ambacho kina ubora mkubwa.

“Sio rahisi kumdhibiti Vinicius Jr sababu ni mchezaji wa kipekee na msumbufu alikuwa anajariu kwa mbinu zote kupambana lakini aliweza kukutana na wachezaji ambao waliweza kumdhibiti kwenye mchezo wetu,”,

Kwenye mchezo huo nyota huyo aliweza kufunga bao moja ilikuwa dk ya 55 na timu yake ya Madrid iliweza kupoteza.