AHMED Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.
Aprili 30,2022 Simba itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Kiungo huyo amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini wanaamini itakuwa kazi kubwa ya kupata ushindi.
“Tumetoka kwenye mashindano ya kimataifa na sasa tupo kwenye hatua nzuri ya kufanya maandalizi dhidi ya Yanga ambao ni wapinzani wetu.
“Ukweli ni kwamba kila mmoja anapenda kuona tunapata pointi tatu lakini tutafanya vizuri na hilo lipo wazi na wachezaji wanajua kwamba tunakwenda kusaka ushindi,”.
Simba ni mabingwa watetezi kwenye ligi wakiwa na pointi 41 wanatarajiwa kukutana na Yanga yenye pointi 54 ikiwa nafasi ya kwanza.