NYOTA ANAYWENDWA NA SIMBA,YANGA MIKONONI MWA WATOZA USHURU

STAA wa Klabu ya Geita Gold ambaye ni namba moja kwa utupiaji ndani ya timu hiyo anatajwa kuwa kwenye rada za watoza ushuru wanaopiga mpira kodi,mpira mapato Klabu ya KMC.

Ni George Mpole ambaye ni mshambuliaji namba moja ndani ya Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro.

Kibindoni katupia mabao 10 ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 na anatajwa pia kuwa kwenye rada za vigogo wa Kariakoo, Simba na Yanga ambao wanawania saini yake.

Pia nyota huyo aliwahi kutajwa kuhitajika na mabosi wa Azam FC ili kuweza kuwa naye kwa msimu ujao katika majukumu mapya.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara aliweka wazi kwamba usajili ambao wataufanya kwa ajili ya msimu ujao ni mkubwa na utakuwa wa kipekee.