HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa Henock Inonga beki wa Simba ni moja ya wachezaji wazuri lakini wanapenda kucheza na jukwaa.
Inonga ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Pablo Franco ndani ya Simba anapewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Aprili 30 mbele ya Yanga.
Manara amesema:“Inonga ni beki mzuri lakini sijui shida yake inakuwa nini pia anapenda kucheza na akili za fans kuliko majukumu yake, kwa beki mzuri hawezi kufanya hivyo.
“Kuna wakati anafanya jambo ili anufaishe mashabiki hivyo kama ataweza kucheza mpira atafanya vizuri pale akicha kucheza na jukwaa,”.
Inonga alikuwa beki kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa wa mzunguko wa kwanza walipotoshana nguvu ya bila kufungana.