SHOMARI Kapombe beki wa kazi ngumu kimataifa mwenye mabao mawili na pasi mbili amesema kuwa alimwambia kipa wa Orlando Pirates, ‘Maharamia’ ninakufanga na kweli alimfunga.
Kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali uliochezwa nchini Afrika Kusini wakati wa mapigo ya penalti baada ya jumla ya mabao ya kufungana kwa Simba kuwa 1-1, kipa wa Orlando Pirates,Richard Ofori alionekana akimfokea Kapombe.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kapombe amesema kuwa kipa huyo alikuwa akimpiga mkwara kwa kuwa walipokutana Dar alimfunga kwa penalti.
“Kikubwa aliniambia kwamba nilimfunga Dar sitaweza kumfunga tena kule kwao, nikamwambia kwamba ninaweza kukufunga na mwisho nikamfunga kwa penalti kisha nikamuuliza unasemaje?
“Kuhusu kurejea na kupokewa na mashabiki katika hilo ninafurahia mashabiki kuwepo hapa na tangu mashindano yanaanza walikuwa pamoja nasi na unaona kwamba tumetolewa lakini mashabiki wamekuja kutupokea tunafarijika.
“Hatukutaka kupata matokea haya kuanzia mchezo wa kwanza mpaka tumefika hatua ya robo fainali sina cha kuwaambia zaidi ya kusema asante.
“Sikutegemea kuona kwamba ingekuwa hivi unaweza kusema kwamba kila kitu kilikuwa kizuri na kuja kwao hapa mashabiki kwetu ni furaha na kila mmoja anapenda kuona tunasonga mbele lakini haikuwa hivyo,” amesema Kapombe.