HASSAN BUMBULI:LENGO LETU NI UBINGWA

HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa lengo lao ni kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu na kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba wanaamini kwamba watapata matokeo.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu leo kwenye kipindi cha Global Radio amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 30.

Bumbuli amesema:”Tunajua kwamba mchezo wetu ujao utakuwa mgumu na tutafanya kazi kubwa kusaka ushindi kwa kuwa hawa wachezaji wa timu zote mbili wanahitaji ushindi.

“Ambacho tunakifanya ni maandalizi na timu yetu ilianza maandalizi kwa muda mrefu kwenye mechi hii tayari wachezaji wapo kwenye kambi wakiendelea na mazoezi.

“Ukweli ni kwamba tunahitaji ubingwa wa ligi na tunajua kwamba mchezo wetu ujao utakuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi,”.