YANGA WAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA SIMBA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba unazitaka pointi tatu za watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ni Aprili 30,2022 Yanga inatarajiwa kumenyana na Simba kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kuhusu umuhimu wa mchezo huo na wataingia uwanjani kwa nidhamu lakini wanahitaji ushindi.

“Tunakwenda kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba ambao utakuwa ni mchezo mgumu lakini ambacho tunakihitaji ni pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo.

“Kuanzia wachezaji na benchi la ufundi kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu huo ambao ni muhimu kuona kwamba tunapata ushindi,”amesema.

Mzunguko wa kwanza watani hawa wa jadi Desemba 11,2021 walitoshana nguvu bila kufungana.