KIKOSI cha Simba Queens leo kimechapwa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake.
Ilikuwa ni mchezo mkali ndani ya Uwanja wa Mkapa ambapo timu zote zilianza kwa kushambulia.
Ilikuwa dk ya 5 Simba Queens walipata pigo baada ya beki wao tegemeo Singano Julieth kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea faulo Clara Luvanga wa Yanga Princess.
Bao pekee la ushindi kwa Yanga Princes lilifungwa na Luvanga akiwa nje ya 18 na kuwafanya Simba Queens kupoteza pointi tatu jumlajumla.
Ushindi huu kwa Yanga unawafanya waweze kuifunga Simba kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2021/22 na kufikisha pointi 35.