SIMBA:TUTAJARIBU KUSHINDA LEO KIMATAIFA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa leo watajaribu kushinda mbele ya Orlando Pirates kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Saa 1:00 usiku, wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ambao ni Simba wana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Orlando Pirates.

Huu ni mchezo wa hatua ya robo fainali ukiwa ni wa pili baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Shomari Kapombe.

Pablo amesema:”Tutajaribu kushinda kwenye mchezo wetu muhimu na tunatambua kwamba ushindani utakuwa mkubwa, kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo wa leo hivyo tutajaribu, kushinda”.

Rally Bwalya, kiungo wa Simba amesema wachezaji wapo tayari na wanahitaji kupata ushindi.

“Tupo tayari na tunajua umuhimu wa mchezo huu kwa kuwa tunahitaji kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho,”.