LIGI ya Beach Soccer inayodhaminiwa na Global Radio na Global TV Online jana April 23 imeendelea katika Viwanja vya Coco Beach kulikuwa na michezo mitatu ya kundi A na leo tena inatarajiwa kuendelea.
Mchezo wa kwanza ulikamilika na Savanah Boys iliibuka na ushindi wa mabao 6-4 Ilala FC.
Mchezo wa pili Kundi A ulikuwa na ushindani na mwisho ubao ulisoma PCM 2- 6 Friends Of Mkwajuni
Mchezo wa tatu na wa mwisho katika viwanja vya Coco Beach ilikuwa Vigunguti 6- 3 Dar Centre.
Mashabiki wengi walijitokeza katika Fukwe Coco Beach ambapo Boniphace Pawasa, Mratibu wa Mashindano haya yanayodhaminiwa na Global TV Online na Global Radio amesema ulinzi ni wa uhakika.
“Mashabiki wanajitokeza kwa sasa hilo ni jambo jema na ulinzi ni mkubwa hivyo Jumapili ligi itaendelea,” amesema.