SIKU YA 62 BILA KUFUNGWA KWA LUSAJO

NYOTA wa Namungo, Relliats Lusajo leo anafikisha siku ya 62 bila kufunga bao ndani ya mechi za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Nyota huyo mzawa alianza kwa kasi matata na aliweza kuwa namba moja kwa muda kwa watupiaji wa ligi alipofikisha mabao 10 kibindoni.

Mara ya mwisho Lusajo kufunga ilikuwa ni Februari 21,2022 Uwanja wa Ilulu mbele ya Mbeya City ambapo alifunga bao lake la 10 kwenye ligi.

Leo wanatarajiwa kumenyana na Yanga ambao ni vinara wa ligi kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Ni mabao 11 anayo kinara wa utupiaji ndani ya ligi ambaye ni Fiston Mayele na ana pasi tatu za mabao.