JULIO:MAYELE NI POMBE,ATATUFUNGAJE SASA AKISHALEWA

IKIWA leo wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga v Namungo, Kocha Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo,’Julio’ amesema watapambana kufanya vizuri.

Julio amebaainisha kwamba haoni sababu ya kuhofia mchezaji mmoja ama timu kiujumla kwa kuwa wamejipanga kufunga na kupata pointi tatu.

Amemtaja Mayele kwamba hawezi kuwafunga leo kutokana na jina lake kuwa na maana ya Pombe kwa lugha ya kihehe.

“Mayele,(Fiston) mi Mhehe, Mayele kihehe maana yake Pombe,sasa maana yake hiyo Pombe tayari ameshalewa sasa sijui atatufungaje.

“Tupo tayari kwa ushindani na tumepjipanga vizuri tukutane uwanjani na ninasema kwamba twende tukashindane,”

Mayele ni mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga na ligi kiujmla akiwa ametupia mabao 11 na pasi tatu za mabao.

Kwa upande wa Namungo ni Relliats Lusajo yeye amefunga mabao 10 na pasi mbili za mabao.