KIUNGO mkabaji wa Kiyovu ya Rwanda, Mrundi, Ismail Nshimiyimana ‘Pitchou’, amefunguka kuwa, haitakuwa shida kwake kama ikitokea anapata nafasi ya kucheza sambamba na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei ToTo’ kutokana na uwezo mkubwa alionao licha ya kuheshimu uwepo wa Mganda, Khalid Aucho.
Pitchou ametoa kauli hiyo kufuatia wiki iliyopita kufuatwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, akiwa na Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ambao walikuwa nchini Rwanda kwa ajili ya kumfuatilia kiungo huyo sambamba na pacha wake Abed Bigirimana ambao wote wanachezea Kiyovu.
Pictchou alisema kuwa amekuwa akiifuatilia timu hiyo katika mechi zake za ligi lakini amekuwa akitamani kucheza pomoja na Fei Toto kutokana na uwezo mkubwa alionao akicheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji kwa kuamini watafanya makubwa.
“Nadhani kwangu ikitokea nakuja Yanga natamani kuona napata nafasi ya kucheza na Fei kwa sababu kwanza amekuwa na ubunifu lakini anajua wakati gani wa kufanya maamuzi akiwa na mpira, nadhani italeta utofauti mkubwa kwa kuwa nitakuwa katika eneo la chini na yeye akiwa juu tutafanya mambo makubwa,”