YANGA YAPANIA KUIVURUGA SIMBA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba utawavurugia hesabu za kutwaa pointi tatu Simba watakapokutana Aprili 30 kwa kuwafunga mapema ili kukamilisha hesabu.

Vinara hao wa ligi wakiwa na pointi 51 wamewaacha wapinzani wao Simba kwa pointi 10 na timu zote mbili zimecheza mechi 19.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanajua kwamba mchezo huo upo na wao ambacho watakifanya ni kushinda mchezo huo.

“Tunamchezo dhidi yao hao ambao tumewaacha kwa pointi 10, (Simba) ambacho tutakifanya ni kuvuruga hesabu zao za kuweza kupata pointi tatu kwenye mchezo huo wa ligi.

“Kwa mashabiki ninawaambia kwama waanze kujiaandaa mapema kuelekea mchezo huo hasa kuona namna ambavyo tutafanya kwani kila kitu kinakwenda sawa na morali ya wachezaji ipo juu,” amesema Bumbuli.

Zimebaki siku 10 kabla ya watani wa jadi kuweza kukutana Uwanja wa Mkapa,Aprili 30,Uwanja wa Mkapa.