TANZANIA BADO INA KAZI KUBWA YA KUFANYA AFCON

BAADA ya kupangwa kwenye hatua ya makundi ya kufuzu Afcon ikiwa kundi F, mwandishi wa masuala ya michezo Tanzania, Marco Mzumbe amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kwa Tanzania.

Ni kundi F ambalo Tanzania imepangwa ikiwa na timu za Algeria,Uganda na Niger ikiwa ni kwa ajili ya kufuzu AFCON 2023.

Mzumbe amesema ukiwatazama Algeria katika timu za ukanda wa Afrika ipo daraja A.

“Sisi tupo daraja la tatu na timu nyingine kama Somalia hivi ukiwatazama Niger wao wamepanda, kwa hiyo ambacho kinatakwa kufanyikahapo ni jambo moja la kujitoa na kufanya juhudi.

“Madaraja ya nne kama Somalia hawa nao wapo ila Niger hata sisi wametupita kwenye viwango, ukitazama kwenye makaratasi sisi tunaonekana kuwa ni vibonde, ambacho kinatakiwa kufanyika ni maandalizi mazuri.”,